Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP yawapelekea msaada wa dharura wa chakula Allepo

WFP yawapelekea msaada wa dharura wa chakula Allepo

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula WFP limepeleka msaada wa chakula kwa watu 28,000 mjini Aleppo kwa siku chache zijazo baada ya kupata taarifa za upungufu wa chakula,g esi na umeme vilivyosababishwa na mapigano yanayoendelea kwa wiki kadhaa sasa. Shirika hilo linasema hali ya kibinadamu inazidi kuzorota na mahitaji ya chakula yanaongezeka kwa haraka huku mapigano makali yakiingia wiki ya pili na kuwalazimisha watu 20,000 kufunga virago na kukimbia mji huo. George Njogopa na taarifa kamili.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)