Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vita vyashika Kasi Syria, Serikali yatumia Ndege za Kivita na Wapinzani Silaha Nzito:UNSMIS

Vita vyashika Kasi Syria, Serikali yatumia Ndege za Kivita na Wapinzani Silaha Nzito:UNSMIS

Mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Syria unasema waangalizi wa kimataifa wameshuhudia ndege za kivita zikishambulia kwenye mji mkbwa kabisa wa Syria ambako mapigano yametanda kwa karibu wiki mbili sasa. Msemaji wa mpango huo UNSMIS Susan Ghosheh ameelezea hofu yake kuhusu hali mjini Aleppo. Amesema jana kwa mara ya kwanza wameshuhdia mashambulizi hayo ya anga na pia sasa wamethibitisha kwamba wapinzani wanamiliki silaha nzitonzito vikiwemo vifaru. Bi Ghosheh akitoa taarifa Jumatano amesema kwa sasa kuna upungufu mkubwa wa chakula, maji, na gesi.

(SAUTI YA SAUSAN GHOSHEH)