Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bunge la Somalia lapitisha Katiba Mpya

Bunge la Somalia lapitisha Katiba Mpya

Viongozi wa serikali ya mpito ya Somalia wanaokutana Moghadishu wamepitisha kwa wingi wa kura katiba mpya ya nchi hiyo ambayo inafungua mlango wa kuchaguliwa kwa serikali mpya mwezi huu. Jumla ya wabunge 825 walikuwa wakijadili kuhusu katiba hiyo kwa juma zima na wabunge 621 wamepiga kura ya ndiyo, 13 wamepinga na 11 hawakupiga kura kabisa.

Katiba hiyo inajumuisha vipengee ya haki binafsi na inaielekeza nchi katika serikali inayojmisha wote. Katiba hiyo mpya pia inaweka bayana kwamba Sharia za Kiislam ndio msingi wa Somalia, pia inaaelezea haki ya toaji mamba kwa kuokoa maisha ya kina mama na kpiga marufuku ukeketaji dhidi ya wasichana na wanawake Somalia.Kwa mujibu wa mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa nchini humo balozi Augstine Mahiga huu ni mwanzo wa ukurasa mpya Somalia, na viongozi wanathibitisha kuheshimu mchakato wa kisiasa nchini humo.

(SAUTI YA BALOZI MAHIGA)

Chini ya mpango unaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa kiongozi mpya wa Somalia anapaswa kuchagliwa Agosti 20 mwaka huu. Somalia imekuwa bila serikali imara tangu mwaka 1991 alipopinduliwa Siad Barre.