Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ghasia zaidi zasababisha idadi ya Wasyria wanaokimbilia Usalama wao Kupanda

Ghasia zaidi zasababisha idadi ya Wasyria wanaokimbilia Usalama wao Kupanda

Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR, limeelezea wasiwasi wake kuhusu idadi kubwa zaidi ya raia wa Syria walolazimika kuhama makwao, hasa kufuatia kuongezeka kwa machafuko katika mji wa Aleppo, ambao ndio mji wenye idadi kubwa zaidi ya watu nchini humo.

Msemaji wa UNHCR, Melissa Fleming amesema kuwa shirika hilo na wadau wengine wamekuwa wakishuhudia maelfu ya watu wenye uoga mwingi wakitafuta makazi salama kwenye shule, misikiti na majengo ya umma. Amesema afisi ya UNHCR mjini Aleppo inashindwa kutekeleza majukumu yake kwa sababu za kiusalama .

Shirika hilo pamoja na wadau wengine wameonya pia kuwa kutokuwa na ufadhili wa kutosha kutabana uwezo wao kuitikia mahitaji muhimu ya wakimbizi.

(SAUTI  YA MELISSA FLEMING)

Amesema kuwa afisi ya UNHCR katika mji wa Damascus sasa hivi ina asilimia 50 tu ya uwezo wa kutimiza majukumu yake kwa sababu ya vizuizi vya kiusalama.