Wanawake wengi katika nchi za Jumuiya ya Ulaya wako hatarini kupoteza kazi

Wanawake wengi katika nchi za Jumuiya ya Ulaya wako hatarini kupoteza kazi

Ripoti moja iliyotolewa na shirika la kimataifa imesema kuwa wanawake ambao wanafanya kazi katika sekta za umma walioko katika nchi zilizoko kwenye Umoja wa Jumuiya ya Ulaya wanakabiliwa na hali ngumu iliyosababishwa na tukio la kupunguza ajira na kuondoka kwa marupurupu ya ujira.

Ripoti hiyo iliyochapishwa na kamishna ya kazi ya Jumuiya ya Umoja wa Ulaya inaonyesha kiwingu cha kupoteza ajira kinachowaandama wanawake katika nchi zilizoko kwenye Jumuiya hiyo kutokana na sera kali zinazotekelezwa.

Imeonya ripoti hiyo juu ya kile ilichokiita uwezekano wa kuanguka ustawi na mafanikio yaliyofikiwa iwapo mwenendo huo hautarekebishwa. Pia imejadilia eneo la kijinsia ambalo imesema kuwa kutokana na sera kali wanawake wengi ndiyo wanaathirika.

--