Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kamishina Guterres aitembelea nchi ya Burkina Faso

Kamishina Guterres aitembelea nchi ya Burkina Faso

Kamishina mkuu wa shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa Antonio Gutteres anaanza ziara ya siku tatu nchini Burkina Faso hii leo kujionea hali ya zaidi ya wakimbizi 100,00 kutoka nchini Mali na athari zake kwa mataifa jirani.

Tangu kuanza kwa mzozo mwezi Junuari zaidi ya watu 250,000 kutoka Mali wamevuka mpaka na kuingia nchini Burkina Faso, Mauritania na Niger huku watu 167,000 wakiwa ni wakimbizi wa ndani nchini Mali. Kwa sasa inakadiriwa kuwa zaidi ya watu milioni kumi wanahitaji msaada wa dharura hali iliyochangiwa na uhaba wa mvua , mavuno duni , kupanda kwa bei ya vyakula na mizozo. Alice kariuki na taarifa kamili.

(SAUTI YA ALICE KARIUKI)