Wakimbizi wanahitaji msaada ya dharura Ivory Coast:UM

31 Julai 2012

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki ya wakimbizi wa ndani amesema kuwa wakimbizi wa ndani nchini Ivory Coast wanahitaji suluhisho likiwemo ya uhakika kwa usalama wao ili waweze kujenga upya maisha yao. Chaloka Beyani ambaye amefanya ziara nchini Ivory Coast tangu tarehe 23 hadi 31 mwezi huu amesema kuwa huku serikali ikiwa imepiga hatua katika kutekelezwa kwa sheria nchi humo na kuwasaiadia wakimbizi wa ndani kurejea makwao wakimbizi hao wanahitaji usaidizi na na usalama.

Idadi ya wakimbizi wa ndani nchini Ivory Coast ilikadiriwa kuwa wakimbizi milioni moja wakati wa mzozo wa uchaguzi mwezi machi mwaka 2011 baada ya wakimbizi wa ndani waliolazimika kuhama makwao mwaka 2001 kulazimishwa kuhama tena mwaka 2011. Beyani ameitaka jamii ya kimataifa kundelea kuunga mkono huduma za kibinadamu na mabadiliko kwenye serikali katika sekta muhimu na katika kutafutiwa makao watu waliohama makwao.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud