Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ahimiza nchi za G20 zifanye Mipango Inayouiana na Matokeo ya Rio+20

Ban ahimiza nchi za G20 zifanye Mipango Inayouiana na Matokeo ya Rio+20

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amesema kushirikisha matokeo ya mkutano wa Rio+20 katika ratiba za nchi za G20 ni muhimu katika kufikia maendeleo endelevu. Akilihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu mkutano wa G20, Bwana Ban amesema, inapasa uwepo ushirikiano katika kuweka ajenda kamilifu ya maendeleo baada ya mwaka 2015.

Bwana Ban amesema kuwa anatangaza leo jopo la viongozi wenye hadhi ya juu, likiongozwa na marais wa Indonesia na Liberia na Waziri Mkuu wa Uingereza, ambalo linatarajiwa kubuni malengo ya maendeleo endelevu (SDGs). Jopo hilo la watu 27, litafanya mkutano wake wa kwanza mnamo mwezi Septemba, wakati wa Mkutano wa marais na viongozi wa Baraza Kuu. Ametoa wito kwa mataifa ya G20 kuunga mkono mfuko wa kulinda mazingira, yaani Green Climate Fund, na kuyashukuru kwa juhudi zao za kuhakikisha lishe kwa wote.