Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama lataka suluhu Guinea Bissau

Baraza la Usalama lataka suluhu Guinea Bissau

Baraza la Usalama zimetolewa mwito pande za kisiasa nchini Guinea Bissau kuanzisha majadiliano ya mezani ili kutanzua mkwamo unaendelea kuliandama taifa hilo ambalo liko Magharibi mwa Afrika.

Baraza hilo limeweka zingatio likitaka kuanzishwa kwa majadiliano ya kitaifa na kurejesha utawala wa kikatiba pamoja na kuanzisha sura ya maridhiano kwa pande zote.

Katika taarifa yake, baraza hilo limeunga mkono juhudi zinazoendelea kutolewa na Jumuiya ya kikanda ya eneo la afrika magharibi ECOWAS ambayo inaendesha ushawishi wenye lengo la kumaliza mkwamo huo uliopaliliwa na kundi la askari waliozima madaraka ya kiraia.

Tangu kujipatia uhuru wake mwaka 1974 toka kwa Ureno, askari katika taifa hilo mara kwa mara wamejihusisha na vitendo vya upokaji madaraka toka kwa utawala wa kiraia.