Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Benki ya Dunia yaonya kuhusu Kupanda kwa Bei ya Vyakula

Benki ya Dunia yaonya kuhusu Kupanda kwa Bei ya Vyakula

Benki ya dunia imeonya kuwa hali ya ukame inayoendelea kushuhudiwa nchini Marekani na hali zilizopo kwenye nchi zingine zinazozalisha nafaka na kupanda ya bei ya vyakula huenda vikaathiri nchi maskini.

Rais wa benki ya dunia Jim Young Kim anasema kuwa wakati bei ya chakula inapopanda, familia huondoa watoto wao shuleni na kula vyakula nafuu vyenye lishe duni vilivyo na madhara ya muda mrefu yakiwemo ya kisaikolojia kwa mailioni ya watu hasa vijana. Mwaka 2008 bei ya mchele ilipanda zaidi ya mara tatu hali iliyowaathiri pakubwa watu maskini hasa barani Asia.