Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mafuriko yawaua watu 88 Korea Kaskazini na kuwaacha maelfu bila makao

Mafuriko yawaua watu 88 Korea Kaskazini na kuwaacha maelfu bila makao

Gharika la mvua na chamchela yenye jina Khannun kati ya mwezi Julai, imesababisha mafuriko yalowaua watu 88 na kuwaacha maelfu ya wengine bila makao katika majimbo manne ya jamhuri ya Korea Kaskazini. Mvua nyingi ilonyesha siku ya Jumapili imeifanya hali kuzorota zaidi. Serikali ya Korea Kaskazini imezindua mikakati ya dharura ya kuwahamisha watu walioathirika.

Katika majimbo yote yaloathiriwa na janga hili, uchumi na riziki za watu zimeathirika vibaya mno. Serikali ya Korea Kaskazini imetoa wito kwa mashirika ya Umoja wa Mataifa kusaidia katika kukidhi mahitaji ya waathiriwa.