Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Msafara wa UNSMIS Washambuliwa kwa Risasi

Msafara wa UNSMIS Washambuliwa kwa Risasi

Kumeripotiwa shambulizi la risasi kwa msafara wa magari matano ya Waangalizi wa Umoja wa Mataifa nchini Syria, UNSMIS, katika eneo la Talbisa, yapata kilomita 17 kutoka mji wa Homs. Miongoni mwa wasafiri kwenye msafara huo alikuwemo Luteni Jenerali Gaye, Mkuu mpya wa UNSMIS, ambaye amechukuwa wadhfa huo wiki ilopita, akimrithi Meja Jenerali Robert Mood.

Gari la kwanza kwenye msafara huo lilirushiwa risasi tatu na la tatu, ambalo lilikuwa limembeba Jenerali Gaye, likapigwa risasi moja. Hakuna majeraha yoyote yaliyoripotiwa kwa wafanyakazi wa UNSMIS.