Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jordan yafungua Kambi Mpya kwa Wakimbizi kutoka Syria

Jordan yafungua Kambi Mpya kwa Wakimbizi kutoka Syria

Huku watu zaidi wakiendelea kuihama Syria taifa jirani la Jordan limefungua kambi mpya kwa lengo la kuondoa misongamano iliyo kwenye mpaka waliko maelfu ya raia wa Syria. Hadi mwishoni mwa juma lililopita wakimbizi 10,000 wa Syria walikuwa wakiishi kwenye kambi nne zilizo na misongamano kwenye mpaka kati ya Jordan na Syria.

Wakimbizi wengine 1500 wanawasili kila siku kupitia sehemu tofauti za mipaka hasa kutoka kusini mwa Syria Kusini. Wengi wa wakimbizi hawa wamekuwa wakisaidiwa na wanyeji wa Syria lakini kuendelea kuongezeka kwa wakimbizi imekuwa ni changamoto kubwa kwa wenyeji.