Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu 200,000 wakimbia Mapigano Makali katika mji wa Aleppo nchini Syria:UNHCR

Watu 200,000 wakimbia Mapigano Makali katika mji wa Aleppo nchini Syria:UNHCR

Takriban watu 200,000 wamekimbia mapigano makali katika mji wa pili mkubwa zaidi nchini Syria, Aleppo katika siku mbili zilizopita, limesema Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR. Kwa mujibu wa UNHCR, wengi watu waliolazimika kuhama makwao hawajavuka mipaka ya kimataifa, na hivyo kufanya wahudumu wa kibinadam kuwafikia kuwa mgumu hata zaidi.

Msemaji wa UNHCR, Melissa Fleming anasema idadi ndogo ya wakimbizi wamekimbilia Uturuki, lakini wengine wengi hawawezi kwa sababu nyingi, ikiwemo kushindwa kupitia barabara zinazoelekea Uturuki kwa sababu za usalama.

Amesema ni vigumu kujua idadi kamili ya wakimbizi, kwani idadi iliopo ni ile tu ya wale ambao hujiandikisha rasmi. Ameongeza kuwa Shirika la UNHCR sasa limefungua mahema 2,000 kwa makazi ya wakimbizi 5, 000 nchini Jordan, na kuwasifu raia wa Jordan kwa ukarimu wao.

(SAUTI YA MELISSA FLEMING)