Ugonjwa hatari wa Ebola wathibitishwa Kuzuka Uganda, Waua watu 14:WHO

30 Julai 2012

Wizara ya Afya nchini Uganda imetoa taarifa kwa Shirika la Afya Duniani, WHO, kuhusu kuzuka kwa homa hatari ya Ebola katika wilaya ya Kibaale ilio magharibi mwa nchi hiyo. Kati ya visa 20 hadi 25 vimeripotiwa tangu mwanzoni mwa mwezi Julai 2012, ikiwa ni pamoja na vifo 15.

Kisa cha kwanza kilitambuliwa katika familia moja kutoka kijiji cha Nyanswiga, ambapo visa tisa vya vifo vimeripotiwa. Walofariki ni pamoja na muuguzi ambaye alitoa huduma kwa mgonjwa mmoja na mtoto wake wa umri wa miezi minne. Visa tisa vya vifo hivyo kumi na vinne vimetokea katika kaya moja. Uthibitisho wa maabara umefanywa na Taasisi ya Utafiti wa Virusi ya Uganda mjini Entebbe. WHO inasema asilimia 56 ya waathirika wanafariki dunia, ambacho ni kiwango cha juu sana. George Njogopa na taarifa kamili:

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud