Watoto 60,000 huenda wakakosa shule DRC baada ya shule nyingi kuporwa na kuharibiwa:OCHA

30 Julai 2012

Ripoti mpya ilotolewa na shirika la kuratibu misaada ya kibinadam la Umoja wa Mataifa, OCHA na wadau wengine, inasema raia wanaathirika kwa kiasi kikubwa na kuongezeka machafuko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Kwa sababu hii, ripoti inasema takriban watoto 60, 000 huenda wakakosa elimu wakati muhula mpya wa shule ukianza mnamo mwezi Septemba.

Tangu mwezi Aprili mwaka huu, kuzorota kwa hali ya usalama kumewalazimu zaidi ya watu 220, 000 kuhama makwao katika jimbo la Kivu ya Kaskazini. Takriban watu 54, 000 wamekimbilia nchi jirani za Uganda na Rwanda. Monica Morara na taarifa kamili.

(SAUTI YA MONICA MORARA)

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter