27 Julai 2012
Ripoti mpya kuhusu mahitaji ya chakula nchini Zimbabwe inasema kuwa mmoja kati ya watu watano sehemu za vijijini nchini humo ambao ni karibu watu milioni 1.6 watahitaji msaada wa chakula msimu wa njaa unaokuja ikiwa ni asilimia 60 zaidi ya waliohitaji msaada kama huo msimu uliopita.
Hii ni kulingana na utafiti unaokadiria usalama wa chakula nchini Zimbabwe ambao unaondesha kila mwaka na serikali kwa ushirikiano na mashirika ya Umoja wa Mataifa na yale yasiyokuwa ya serikali. Mkurugenzi wa shirika la mpango wa chakula duniani nchini humo WFP Felix Bamezon anasema kuwa kwa sasa shirika hilo na washirika wengine wanajiandaa kuchukua hatua zinazohitajika