Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Takriban watu milioni 1.5 wanahitaji msaada wa kibinadamu Syria:UNICEF

Takriban watu milioni 1.5 wanahitaji msaada wa kibinadamu Syria:UNICEF

Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa, UNICEF limesema takriban watu milioni 1.5 wanahitaji msaada wa kibinadam nchini Syria. Kwa mujibu wa shirika la UNICEF, karibu nusu ya idadi hiyo, ni watoto na vijana barubaru.

Shirika hilo limekuwa likitoa misaada na huduma muhimu kwa mamia ya maelfu ya watoto ndani mwa Syria, licha ya kuongezeka machafuko na hatari kwa madreva na timu za kusambaza misaada. Tangu mwezi Januari mwaka huu, UNICEF na wadau wengine wamewafikia watu 190, 000 na misaada ya kibinadamu, wakiwemo watoto 145, 000.

Baadhi ya misaada inayotolewa ni vifaa vya watoto wachanga, vyakula vya lishe ya juu ya protini, vifaa vya kuchezea, huduma za elimu na ushauri. Patrick McCormick ni mseamji wa UNICEF.

(sSAUTI YA PATRICK MCCORMICK)