Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yatoa wito wa kutaka kulindwa kwa maisha ya raia nchini DRC

UNHCR yatoa wito wa kutaka kulindwa kwa maisha ya raia nchini DRC

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limeelezea kushangazwa kwake na ripoti za dhuluma zinazoendeshwa dhidi ya raia maeneo ya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo kufuatia mapigano ya miezi kadha kati ya serikali na makundi yaliyojihami.

Maelfu ya watu wamelazimika kuhama makwao kwenye mkoa wa Kivu Kaskazini wengi wao wakikimbilia usalama nchini Uganda na Rwanda. Kati ya dhuluma wanazopitia watu hawa ni pamoja na mauaji, ubakaji, uporaji , dhuluma za kingono, kazi za lazima na kuingizwa jeshini kwa lazima. Hali hii imesabisha kuhama kwa watu wengi ndani mwa mkoa huo na kwenda nchi majirani. Andrej Mahecic ni msemaji wa UNHCR.

(SAUTI YA ANDREJ MAHECIC)