Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yarejelea shughuli ya kuwahamisha Wahamiaji raia wa Ethiopia Waliokwama nchini Yemen

IOM yarejelea shughuli ya kuwahamisha Wahamiaji raia wa Ethiopia Waliokwama nchini Yemen

Ndege mbili za shirika la kimataifa la uhamaiaji IOM zinatarajiwa kuondoka nchini Yemen hapo kesho na siku ya Jumanne kuelekea Addis Ababa nchini Ethiopia zikiwasafirisha wahamiaji 554 raia wa Ethiopia. Wahamiaji hao wamekwama kwenye mji ulio kaskazini magharibi mwa Yemen wa Haradha karibu na mpaka na Saudi Arabia.

Mji wa Haradh ni kivukio kwa wahamiaji kutoka pembe ya Afrika wanaosafiri kwenda Saudi Arabia kutafuta ajira, lakini kutokana na sheria kali upande wa Saudi Arbaia wengine huwa wanakwama kwenye mji huo. Maafisa wa kibalozi wa Ethiopia na upande wa uhamiaji nchini Yemen kwa sasa wako Haradh wakitoa stakabadhi za usafiri kwa wahamaiji hao. Jumbe Omari Jumbe ni msemaji wa IOM.

(SAUTI YA JUMBE OMAR JUMBE)