Kampeni dhidi ya Usafirishaji Haramu wa Binadamu yafanyika mjini London

27 Julai 2012

Wageni wanaoingia mji wa London kuhudhuria mashindano ya olimpiki huenda wakakumbana na masanduku makubwa yanayaovutia lakini bunde wanapoingia ndani wao hupata kujionea na kuelewa hali ngumu wanayopitia watu wanaosafirishwa kiharamu.

Masanduku hayo ni sehemu ya kampeni yenye lengo la kutoa hamasisho kuhusu ulanguzi wa binadamu tatizo ambalo linaathiri kila nchi duniani kwa njia moja au nyingine. Huku maelfu ya wanariadha wakiwa London kung’ang’ania medali , kwa kila dakika, kila saa na kila siku wanaume , wanawake na watoto wanalazimishwa kusafiri kote duniani kwa manufaa ya mtu mwingine. George Njogopa na taarifa kamili.

(SAUTI YA  GEORGE NJOGOPA)

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter