UNHCR yawasambazia huduma Waathirika 30,000 wa Machafuko ya Myanmar

27 Julai 2012

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limetoa takwimu zinaoonyesha namna machafuko yaliyojiri katika jimbo la Rakhine, Myanmar walivyoathiriwa na machafuko hayo hata kusababisha watu 30,000 kukosa makazi.

Shirika hilo kwa kushirikiana na wahisani wake limeanzisha juhudi za kusambaza huduma za dharura ikiwemo pia kugawa maturubahi kwa ajili ya kuwasitili waathirika wa machafuko hayo.

Takwimu nyingine zinaonyesha kuwa kiasi cha watu 80,000 walioko katika miji mingine ya Sittwe na Maungdawa nao wamekosa makazi.

Baadhi ya waathirika wamewaambia maafisa wa UNHCR wangependa kurejea nyumbani kuendelea na shughuli zao lakini wanahofia usalama wao.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter