Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

OCHA yahimiza kubadilisha mtazamo ili kuepuka janga la kibinadamu nchini Mali

OCHA yahimiza kubadilisha mtazamo ili kuepuka janga la kibinadamu nchini Mali

Mkurugenzi wa operessheni za Ofisi hiyo ya kuratibu misaada ya kibinadam, John Ging, ametoa wito kwa jamii ya kimataifa kuzingatia hali mbaya ya kibinadam nchini Mali, inatokana na tatizo kubwa la uhaba wa chakula, utapia mlo, idadi kubwa ya watu kulazimika kuhama makwao na kuzorota kwa hali ya usalama kuloenea.

Bwana Ging ambaye amekuwa kwenye ziara ya siku tatu nchini Mali, amesema hali ya kibinadam inaendelea kuzorota kwa kasi, kwa sababu haijaitikiwa ipasavyo. Amesema hali nchini Mali ni ya dharura, ingawa si ya kukata tamaa. Ametoa wito mabadiliko yafanyiwe mtazamo na jinsi misaada ya kibinadam inavyofadhiliwa.

Amesema kuna uwezo wa kuepukana na janga, lakini hiyo ni ikiwa tu fursa za kuongeza juhudi za kukabiliana na matatizo yaliyopo hazitapotezwa. Zaidi ya watu 42, 000 wamelazimika kuhama makwao nchini Mali, au kukimbilia nchi jirani za Niger, Mauritania na Burkina Faso, ambazo pia zinakumbwa na tatizo la njaa.