Bado kuna mkwamo mkubwa kurejea kwenye mazungumzo ya moja kwa moja Mashariki ya Kati:UM

26 Julai 2012

Ripoti zinaonyesha kuwepo kwa mkwamo juu ya ufufuajii wa mazungumzo ya moja moja ya utanzuaji wa mzozo wa mashariki ya kati wakati ambapo mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa kwenye eneo hilo akizidi kuzipa msukumo juhudi zake.

Mjumbe huyo Robert Serry amesema kuwa pamoja na kuendelea kutanda kiwangu cha kiza kwenye ufufuaji wa majadiliano hayo ya moja kwa moja hata hivyo juhudi ya kuyakwamua majadiliano hayo yanaendelea.

Katika taarifa yake mbele ya baraza la usalama mjumbe huyo amesema kuwa pande zote Palestina na Israel bado zinaonyesha mashakaya kurejea mezani.

Kwa mara ya mwisho pande hizo zilirejea kwenye mazungumzo ya moja kwa moja Septemba mwaka 2010 na baada hapo kumejitokeza hali ya mkwamo kutokana na Israel kuendelea na mpango wake wa ujenzi wa nyumba.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter