Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban azitaka Ugiriki, Jamhuri ya zamani ya Yugoslavia kumaliza mzozo wa jina

Ban azitaka Ugiriki, Jamhuri ya zamani ya Yugoslavia kumaliza mzozo wa jina

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuwa kuna haja tena ya msingi kwa Ugiriki na Jamhuri ya zamani ya Yugoslavia ya Mecedonia kumaliza mapema mzozo wa kupatikaja jana rasmi.

Maeneo hayo kwa muda mrefu sasa yameendelea kulumbana juu ya utumiaji wa jina rasmi na hivyo kufanya ustawi wa eneo hilo kuzorota. Ban amezitaka pande zote kufahamu umihimu wa kutanzua mkwamo huo akisisitiza kuwa ni vyema tatizo hilo likatafutiwa ufumbuzi.

Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa kwenye kutanzua mzozo huo Mathew Nimetz amesema yuko tayari kuanzisha juhudi za kukwamua mzozo huo