Muda wa kuhudumu kwa Wataalamu wa Vikwazo vya Silaha kwa Mataifa ya Somalia na Eritrea Waongezwa

26 Julai 2012

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeongeza muda wa kuhudumu  kwa jopo la wataalamu wanaofuatilia kutekelezwa kwa vikwazo vya silaha kwa mataifa ya Somalia na Eritrea. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa liliamua kuongeza muda huo hadi tarehe 25 mwezi Agosti mwaka 2013 kwa jopo ambalo pia linachunguza pia sekta za kifedha na za baharini za mataifa hayo sekta ambazo ni chanzo cha fedha zinaochangia kukiukwa kwa vikwazo.

Kundi hilo la watalaamu pia limetwikwa jukumu la kuchunguzua mifumo yote ya usafiri inayoweza kutumiwa kikiuka vikwazo hivyo. Baraza hilo pia liliamua kuwa vikwazo vya silaha nchini Eritrea havitalenga vyombo vya kujinginga vinavyoingizwa nchini humo na wafanyikazi wa Umoja wa Mataifa , waandishi wa habari na watoa huduma za kibinadamu.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter