Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ushirikiano wahitajika kuwasaidia wakazi wa Camp New Iraq:UNHCR

Ushirikiano wahitajika kuwasaidia wakazi wa Camp New Iraq:UNHCR

Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR, limetoa wito uwepo ushirikiano, subira na ufahamu kwa wote wanaohusika katika juhudi za kutafuta suluhu kwa wakimbizi walioko kwenye kambi iitwayo Camp New Iraq, zamani ikiitwa Camp Ashraf, kaskazini mwa mji mkuu, Baghdad.

Kulinda usalama na kukidhi mahitaji ya watu 3,200 wakazi wa zamani na wa sasa wa kambi hiyo, kunabaki kuwa lengo la msingi la juhudi zinazoongozwa na Umoja wa Mataifa, za kuweza kuifunga hiyo kambi kwa njia ya amani, na kupata suluhu kwa wakazi wake. Kwa sasa, Shirika la UNHCR linakagua mahitaji ya ulinzi wa kila mmoja wa wakazi wa zamani wa Camp New Iraq, wakati wanapohamishiwa kwenye kituo cha muda cha Hurriya.

Shirika hilo pia limetoa wito kwa nchi kuchukua hatua ya haraka kuwakaribisha tena watu ambao walikuwa na uhusiano nazo, au kuwapa makazi mapya na misaada mingine ya kibinadamu. Kambi ya zamani ya Ashraf imekuwepo tangu miaka ya themanini, na wakazi wake wengi wamekuwa wenye asili ya Iran