Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tume ya kulipa fidia ya UM yailipa serikali ya Kuwait dola bilioni 1.3

Tume ya kulipa fidia ya UM yailipa serikali ya Kuwait dola bilioni 1.3

Tume ya kufidia ya Umoja wa Mataifa hii leo imetoa dola bilioni 1.3 kwa serikali ya Kuwait malipo ambayo yanafanywa kutokana na madai sita yaliyosalia yaliyothibishwa kati ya mwaka 1999 na mwaka 2003 na baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.

Madai sita yaliyo kwenye kundi la E ni madai kutoka kwa mshirika na sekta za umma huku mawili yaliyo kwenye kundi la F yakiwa ni kutoka kwa serikali na mashirika ya kiamataifa. Madai hayo hulipwa kutokana na fedha zinazotoka kwa mfuko wa fidia wa Umoja wa Mataifa unaofadhiliwa na asilimia fulani inayotokana na mauzo ya mafuta kutoka Iraq. Asilimia hii ilibuniwa kupitia kwa azimio namba 1483 la baraza la usalama la Umoja wa Mataifa mwaka 2003.