Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kampeni ya kuwachanja watoto dhidi ya Ugonjwa wa Kupooza nchini Afghanistan yaendelea

Kampeni ya kuwachanja watoto dhidi ya Ugonjwa wa Kupooza nchini Afghanistan yaendelea

Karibu wahudumu wa afya 27,000 na watu wanaojitolea walitawanyika kwenye mikoa 16 nchini Afghanistan kwa muda wa majuma mawili yaliyopita katika shughuli ya kuangamiza ugonjwa wa surua na ule wa kupooza kutoka taifa hilo kupitia kwa kampeni inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa.

Wakati huo huo mawaziri wa afya kutoka Afghanistan na Pakistan wamekubaliana kushirikiana kwenye kampeni za kuangamiza ugonjwa wa kupooza ili kuwafikia watoto wanaoishi kwenye mipaka kati ya nchi hizo mbili. Kampeni hiyo iliyozinduliwa na wizara ya afya nchini Afghanistan mapema mwezi huu imewachanja zaidi ya watoto milioni 8 walio na umri wa kati ya miezi tisa na miaka 10 kwa chanjo za ugonjwa wa kupooza na surua. Jason Nyakundi na taarifa kamili.

(SAUTI YA JASON NYAKUNDI)