Hali ya kibinadamu kwa wakimbizi wa Sudan bado ni ya kutia wasiwasi: OCHA

26 Julai 2012

Hali ya usalama katika jimbo la Bahr el Ghazal Kaskazini katika Sudan Kusini bado ingali tete, kufuatia Sudan Kusini kuishutumu jirani wake wa kaskazini, Sudan kurusha bomu katika eneo lake, kwa mujibu wa Afisi ya Kuratibu maswala ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa, OCHA.

Mashirika ya kutoa misaada ya kibinadamu, yamekuwa yakiendelea kuwasaidia wakimbizi 162, 000 wa Sudan walioko kwenye majimbo ya Upper Nile na Unity ya Sudan Kusini. Hata hivyo, mashirika hayo yanakabiliwwa na changamoto ya mvua nzito inayoendelea kunyesha, na hivyo kufanya utoaji wa huduma za kibinadam kuwa mgumu.

Hali ya kibinadamu inatia wasiwasi, hasa ikizingatiwa kuwa watoto wawili kati ya kila kumi walio chini ya miaka mitano, wanafariki kutokana na kuharisha. Jens Laerke ni msemaji wa OCHA

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud