UM watangaza Kupunguza msaada kwa Haiti kwa sababu za ufadhili

25 Julai 2012

Afisi ya kuratibu misaada ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa, OCHA, imetangaza kuwa Umoja wa Mataifa utapunguza kiasi cha fedha za msaada wa kimataifa unazochangisha kwa ajili ya kulisaidia taifa la Haiti kwa sababu mwitikio wa wafadhili haujakuwa wa kutia moyo mwaka huu. Katika mkutano na waandishi wa habari mjini Port au Prince, afisa mkuu wa afisi ya OCHA, Nigel Fischer amesema kuwa, ni wazi kuwa ufadhili wa mahitaji ya kibinadamu yalosalia hautoshi.

Bwana Fischer amesema, bajeti ya awali ya pamoja kwa ajili ya Haiti mwaka wa 2012 ilikuwa dola milioni 231 za Kimarekani, lakini kufikia katikati ya mwaka, ni asilimia 20 tu ya fedha zote zilizoombwa kufanikisha bajeti hiyo zilizopatikana. Hivyo basi, bajeti ya msaada imekatwa kwa kiasi kikubwa na kubakia dola milioni 128 pekee.

Hazina ya msaada wa pamoja kwa ajili ya Haiti inahitaji ufadhili wa kimataifa , ili kuwasaidia watu waloathirika zaidi na matatizo mbali mbali ya kibinadamu. Ingawa ugonjwa wa kipindupindu umwepunguwa, visa 50, 000 vimeripotiwa kufikia Julai mwaka huu, na hivyo unasalia kuwa tishio. Idadi ya watu ambao bado wanaishi kwenye kambi kufuatia tetemeko la ardhi, ni 390, 000.

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter