UNHCR yaomba nchi Jirani za Syria Kuacha mipaka Wazi kwa Wakimbizi

25 Julai 2012

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR, limetoa wito kwa nchi jirani za Syria kuacha mipaka yake wazi kwa ajili watu wa Syria wanaokimbilia usalama wao. Serikali ya Uturuki imeripotiwa kufunga mipaka yake kwa sababu ya kuzorota kwa hali ya usalama. Katika mahojiano na radio ya Umoja wa Mataifa mjini Genevea, msemaji wa UNHCR, Sybella Wilkes, amesema, ingawa Uturuki imefunga mpaka wake kwa usafiri wa wafanyabiashara kutoka pande zote, bado imewekwa wazi kwa ajili ya wakimbizi.

(SAUTI YA SYBELLA WILKES)

Tunavyoelewa, mipaka bado i wazi kwa wakimbizi wa Syria wanaovuka kuingia Uturuki. Tulikuwa na hakikisho kutoka kwa serikali kuwa hivi ndivyo mambo yalivyo. Tunadhani ni muhimu sana kwa mataifa jirani kuacha mipaka yao wazi ili watu wanaotoroka machafuko wapate mahali salama pa kuenda.

Kufikia sasa, UNHCR imeandikisha takriban watu 124, 000, ingawa idadi kamili huenda ni kubwa zaidi.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter