Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nusu ya Waangalizi wa UNSMIS Wameondoka Syria:UM

Nusu ya Waangalizi wa UNSMIS Wameondoka Syria:UM

Nusu ya waangalizi wa Umoja wa Mataifa nchini Syria, UNSMIS, wameshaondoka nchini humo kwa mujibu wa msimamizi wa shughuli za kulinda amani wa Umoja wa Mataifa, Herve Ladsous. Wiki ilopita, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa liliongeza muda wa shughuli za UNSMIS kwa kipindi cha mwisho cha siku 30. Bwana Herve Ladsous amewaambia waandishi wa habari mjini Damascus kuwa, UNSMIS sasa itakuwa na umbo tofauti, linalojumuisha wafanyakazi wachache. Ameongeza kuwa ni lazima machafuko yapunguzwe kwa kiasi kikubwa.

(SAUTI YA HERVE  LADSOUS)