Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahiga Apongeza Hatua za Kutekelezwa Katiba mpya nchini Somalia

Mahiga Apongeza Hatua za Kutekelezwa Katiba mpya nchini Somalia

Mjumbe maalu wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia balozi Augustine Mahiga amekubaliana na mpango uliotumika katika kuwateua wanachama 825 wa kundi linalotarajiwa kukutana juma hili kujadili , kupiga kura na kupitisha katiba mpya ya taifa hilo la pembe ya Afrika.

Mahiga amesema kuwa ni jambo la kutia moyo kutokana na maendeleo yaliyopatikana. Mahiga pia amewashauri wasomali na viongozi wa kisiasa kufanya kila wawezalo kumaliza majukumu yaliyo mbele yao ili kuipeleka Somali mbele. George Njogopa na taarifa kamili.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)