Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban asema kuna uwezekano wa kutumika kwa silaha za kemikali kwenye machafuko ya Syria

Ban asema kuna uwezekano wa kutumika kwa silaha za kemikali kwenye machafuko ya Syria

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelezea shaka shaka yake juu ya uwezekano wa kutumika kwa silaha za kemikali katika mgogoro unaoendelea sasa nchini Syria na ametaka jumuiya ya mataifa kutupia macho eneo hilo ili kufuatilia hali ya mambo..

Ban amesema kuwa wakati hali ya wasiwasi ikizidi kuongezeja juu ya uwezekano wa kutumika silaha hizo itakuwa ni jambo la kulaumiwa na kulaaniwa vikali kama upande wowote kwenye mzozo huo utachukua mkondo huo.

Akizungumza na waandishi wa habari huko Belgrade, Serbia aliko kwenye ziara ya kikazi, Ban amesema jumuiya ya kimataifa inapaswa kuwa macho na kuangazia kwa karibu lolote linaloweza kujitokeza kwenye mzozo huo.

Ama katika hali nyingine mamia ya watu wamepoteza maisha tangu kuzukwa kwa mkwamo huo huku wengine wakiingia mtawanyikoni.