Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wataalam wa FAO na IAEA wahimiza matumizi ya mbolea kwa uzalishaji wa kilimo

Wataalam wa FAO na IAEA wahimiza matumizi ya mbolea kwa uzalishaji wa kilimo

Wataalam wa kilimo wametoa wito kwa wakulima kutumia mbolea za fertiliser pale wanapoweza, ili kuongeza rutuba katika udongo na viwango vya mazao ya kilimo. Wito huu umetolewa kwenye kongamano la wanasayansi, watafiti na viongozi wa ki-sera kutoka zaidi ya nchi themanini, wanaokutana wiki hii mjini Vienna Austria kujadili umuhimu wa kudhibiti udongo katika kuimarisha usalama wa chakula.

Kongamano hilo lilioandaliwa na shirika la nguvu za atomikki, IAEA na Shirika la Kilimo na Chakula Duniani, FAO, lina lengo la kuwasaidia wanasayansi kufahamu ni nini kinachotendeka ndani ya udongo, na hivyo kuwasaidia wakulima kuelewa viwango vinavyofaa vya maji na mbolea katika ukuzaji wa mimea, au kujua aina za mimea inayonawiri vyema katika maeneo ya ukame. Bwana Kizito Kwena ni mtafiti wa maswala ya kilimo kutoka Kenya ambaye yuko kwenye kongamano hilo

(CLIP YA KIZITO KWENA)