IOM yatoa ombi la dola milioni 177 ili kutoa huduma za dharura za kibinadamu

24 Julai 2012

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM linatoa wito wa msaada wa dola milioni 177 zitakazofadhili huduma kwa wahamiaji na wakimbizi wa ndani na waathiriwa wa majanga ya kiasili na mizozo kote duniani. Wito huo wa msaada ni sehemu ya mpango wa Umoja wa Mataifa ulio na lengo la kuhakikisha kuwa mahitaji yote yameratibiwa na washirika wote wa huduma za kibinadamu.

Wito huo pia ni sehemu ya maombi ya kila mwaka ya mashirika yote ya kutoa huduma za kibinadamu chini ya uongozi wa shirika la kuratibu masuala ya kibinadamu la Umoja wa Mataiafa OCHA. Fedha hizo pia zitatumiwa kufadhili miradi kwenye nchi 16 kote ulimwenguni. Jumbe Omari Jumbe ni msemaji wa IOM

(SAUTI YA JUMBE OMARI JUMBE)

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter