Pillay alaani shambulizi kwenye kambi ya wakimbizi wa ndani nchini Ivory Coast

24 Julai 2012

Mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Navi Pillay amelaani shambulizi kwenye kambi ya Nahibly inayowahifadhi wakimbizi wa nadani karibu na mji Duekoue nchini Ivory Coast Ijumaa iliyopita ambapo karibu watu saba waliuawa, 67 wakajeruhiwa na pia kambi hiyo ikateketezwa kabisa hali iliyowalazimu watu 5000 kukimbilia usalama wao. Kundi la uchunguzi kutoka Ukoja wa Mataifa linapelekwa eneo hilo kwa uchunguzi ambao uutachunguzi ambao utachukua siku kumi. George Njogopa na taarifa kaimili

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)

Nalo Shirika la Kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limeelezea masikitiko yake kutokana na ripoti za shambulizi kwenye kambi ya Nahibly. UNHCR sasa inautaka utawala wa nchi hiyo kuwapa usalama waliolazimika kutoroka kambi baada ya shambulizi hilo.

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter