Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zaidi ya watu milioni moja wakabiliwa na tatizo la chakula nchini Senegal: WFP

Zaidi ya watu milioni moja wakabiliwa na tatizo la chakula nchini Senegal: WFP

Zaidi ya watu milioni moja wanakabiliwa na tatizo la chakula nchini Senegal, kwa mujibu wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani, WFP. Katika operesheni zake nchini Senegal, WFP inalenga kuwasaidia watu 862, 000 wakati wa uhaba wa chakula kati ya misimu ya mavuno. Katika eneo la Kolda, WFP imetoa vocha zenye thamani ya dola 40 kwa wasimamizi wa familia 1, 000. Kwa kawaida, wanawake huachwa wajane kwa sababu ya mapigano Casamance, na hivyo kubaki wakilinda familia za kati ya watu 20- 30. Elisabeth Byrs ni msemaji wa WFP.

(SAUTI YA ELIZABETH BYRS)

Aidha, Shirika la WFP linasema limetoa msaada kwa takriban watu milioni 6 kati ya mwezi Januari na Mwezi Juni katika eneo la Sahel, kwa kuwapa fedha za kununua chakula na chakula cha ziada kwa jumla, pamoja na kile kichowalenga hasa akina mama na watoto. Mataifa yalosaidiwa kufikia sasa ni Niger, Chad, Mali, Senegal, Burkina-Faso, Mauritania, Cameroon na Gambia. Nchini Mali pekee, watu 550, 000 wamepewa msaada. Shirika la WFP linapanga kuwasaidia hadi watu milioni 10 katika eneo zima, ingawa bado lina uhaba wa dola milioni 373.