Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM Walaani Mashambulizi ya bomu nchini Iraq

UM Walaani Mashambulizi ya bomu nchini Iraq

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Iraq (UNAMI), umelaani vikali mashambulizi mabaya ya bomu ambayo yamewaua watu wengi na kuwajeruhi wengine zaidi.

Naibu mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya kisiasa, Gyorgy Busztin, ametaja viwango vya ghasia na umwagaji damu nchini Iraq kama vya kufadhaisha.

Wimbi la ghasia lilizuka siku ya Jumapili, na kwa mujibu wa duru za habari, zaidi ya watu 100 wamepoteza maisha yao. Bwana Busztin amesema wahalfu waliopanga na kutekeleza mashambulizi hayo, ni lazima wawajibike kisheria.