Mfuko wa Kimataifa waonyesha Manufaa kwenye Vita dhidi ya Ukimwi

23 Julai 2012

Mfuko wa kimataifa wa kupambana na ugonjwa wa ukimwi , kifua kikuu na malaria umetangaza matokeo mapya hii leo yanayoonyesha kuongezeka kwa matibabu ya ugonjwa wa ukimwi na kuzuia maambukizi ya kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto. Matokeo hayo yanaonyesha kuwa watu milioni 3.6 wanaoishi na virusi vya ukimwi kwa sasa wanapata matibu kupitia programu zinazofadhiliwa na mfuko huo ikiwa ni ongezeko la watu 600,000 tangu mwisho wa mwaka 2010. Kwa ujumla maisha ya watu milioni 8.7 yameokolewa na programu zinazofadhiliwa na mfuko wa kimataifa tangu kubuniwa kwake mwaka 2002 zikiwa ni pamoja na takwimu hadi mwezi Juni mwaka 2012. Mafanikio yaliyopatikana kwenye utoaji wa matibu dhidi ya ugonjwa wa ukimwi kwenye nchi zinazoendelea yametokana na jitihada za watoa huduma za afya kwenye nchi zenye mizigo mizito ya ugonjwa huo.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter