Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNRWA yahofia Wakimbizi wa Kipalestina waliomo nchini Syria

UNRWA yahofia Wakimbizi wa Kipalestina waliomo nchini Syria

Shirika la Umoja wa Mataifa linawasaidia wakimbizi wa Kipalestina, UNRWA, limeelezea hofu yake kuhusu kuzorota zaidi kwa hali nchini Syria, ambako takriban wakimbizi nusu milioni wa Kipalestina wamekuwa wakiishi.

Shirika la UNRWA pia limeelezea hofyu yake kuhusu usalama wa wafanyakazi wake na ule wa maeneo na vifaa vyake vya huduma, hasa katika mji mkuu Damascus. UNRWA ina maeneo katika kambi tisa rasmi nchini Syria, na tatu zisizo rasmi, na kambi ya Yarmouck ya Damascus ndiyo kubwa zaidi, ikiwa na wakimbizi 150, 000 wa Kipalestina.

Msemaji wa UNRWA, Chris Gunness amesema kuzorota kwa hali ya usalama kumefanya uwezo wa UNRWA kuwafikishia huduma muhimu wakimbizi wa Kipalestina kuwa mgumu.

(SAUTI YA CHRIS GUNNESS)