Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakuu wa Kampuni Maarufu Watoa Wito kwa Mataifa Kukomesha Vikwazo vya Usafiri wa watu walio na HIV

Wakuu wa Kampuni Maarufu Watoa Wito kwa Mataifa Kukomesha Vikwazo vya Usafiri wa watu walio na HIV

Wakurugenzi wa kampuni maarufu zaidi duniani, zikiwemo Levi Strauss, Coca-Cola, Johnson & Johnson, NBA na Virgin Unite, wametoa wito kwa nchi 46 ziondoe vikwazo vya usafiri kwa watu wanaoishi na virusi vya HIV.

Zaidi ya wakuu wa kampuni 20 wametia saini azimio la kuahidi kupinga vikwazo vinavyohusishwa na HIV katika kuingia, kuishi au kupata makazi ya kudumu, wakisema sheria na sera kama hizo si tu za kibaguzi, bali pia ni mbaya kwa biashara.

Ahadi hiyo imewekwa mnamo siku ya Jumapili, wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kimataifa wa 19 kuhusu HIV na UKIMWI, unaoendelea mjini Washington Marekani, ambako zaidi ya watu 30, 000 kutoka nchi 200 wanakutana kati ya Julai 22 na 27.

Mkutano huo unafanyika Marekani kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 22, kwa sababu Rais Barack Obama aliondoa vikwazo kwa wasafiri walio na HIV. Mwaka huo huo, Uchina pia iliondoa vikwazo kama hivyo.

Akizungumza na redio ya Umoja wa Mataifa, Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya masuala ya HIV na UKIMWI katika Umoja wa Mataifa, Michel Sidibe, amempongeza Rais Obama kwa uamuzi huo

(SAUTI YA MICHEL SIDIBE)