Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wataalam wapendekeza Mabadiliko kwa Mwongozo wa UM wa Kuwalinda Wanunuzi:UNCTAD

Wataalam wapendekeza Mabadiliko kwa Mwongozo wa UM wa Kuwalinda Wanunuzi:UNCTAD

Wataalam wa kamati maalum ya Umoja wa Mataifa wamependekeza kuwa mwongozo wa Umoja wa Mataifa kuhusu kuwalinda wanunuzi unafaa kufanyiwa mabadiliko. Hayo ndiyo matokeo ya mkutano wa wataalam hao 300, uliofanyika katika makao makuu ya Kamati ya Umoja wa Mataifa kuhusu Biashara na Maendeleo, UNCTAD, kati ya Julai 12 na 13.

Mkutano huo uliowajumuisha wataalam kutoka mashirika ya kitaifa ya kuwalinda wanunuzi, halmashauri za mashindano ya kibiashara na wawakilishi wa umma, ulizingatia uhusiano wa mashindano wa kibiashara na sera zinazowahusu wanunuzi na kulinda haki zao.

Mkutano ulizingatia zaidi ulinzi wa wanunuzi katika mazingira ya mdororo wa uchumi, na kuangazia masuala mengine kama vile maendeleo ya hivi karibuni ya biashara kwenye mtandao wa internet, na aina nyingine za teknolojia.

Mkutano huo ulisisitiza umuhimu wa kuufanyia mabadiliko mwongozo wa Umoja wa Mataifa, ili kuona unaafikiana vipi na mahitaji ya soko la sasa. George Njogopa na taarifa kamili.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)