Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Udongo Bora kwa Chakula Bora:FAO na IAEA

Udongo Bora kwa Chakula Bora:FAO na IAEA

Wanasayansi, watafiti na viongozi wa ki-sera kutoka zaidi ya nchi themanini wanakutana wiki hii mjini Vienna Austria kujadili umuhimu wa kudhibiti udongo katika kuimarisha usalama wa chakula.

Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki, IAEA, likishirikiana na Shirika la Shirika la Kilimo na Chakula Duniani, FAO, lina idara inayotumia mbinu za kinyuklia kufanya utafiti katika mienendo ya udhibiti bora wa udongo.

Mbinu hizi huwasaidia wanasayansi kufahamu ni nini kinachotendeka ndani ya udongo, na hivyo kuwasaidia wakulima kuelewa viwango vinavyofaa vya maji na mbolea katika ukuzaji wa mimea, au kujua aina za mimea inayonawiri vyema katika maeneo ya ukame.

Mataifa wanachama wa IAEA, hasa yale yanayoendelea, hujulishwa kuhusu ujuzi na mbinu hizi. Kongamano hilo linalofanyika kati ya Julai 23 na Juali 27, litaangazia pia udhibiti wa udongo kwa ajili ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.