Ushirikiano wa Umma na Sekta ya Kibinafsi ni muhimu katika Kukabiliana na HIV:ILO

23 Julai 2012

Mkuu wa mpango wa Shirika la Ajira Duniani kuhusu HIV na maeneo ya ajira, Alice Ouedraogo, ametoa wito kuhusishwa zaidi kwa sekta ya kibinafsi katika juhudi za kimataifa za kukabiliana na HIV na UKIMWI.

Akizungumza wakati wa mkutano wa kimataifa wa kumi na tisa kuhusu UKIMWI unaoendelea mjini Washington Marekani, Bi Ouedraogo amesema hatua ikichukuliwa kwenye maeneo ya ajira, inazisaidia kampuni kuelewa suala la HIV vizuri zaidi, na hivyo kuchagiza hatua zaidi hata nje ya mazingira ya ajira, katika mbinu ya ushirikiano wa umma na sekta binafsi. Amesema mpango kama huo una uwezo wa kuwafikia wote wanaohusika katika uzalishaji na ununuzi wa bidhaa au huduma na ujumbe wa kuzuia maambukizi na matibabu.

Ametaja umuhimu wa mipango ya kukabiliana na HIV na UKIMWI katika mazingira ya ajira na kutaka zitekelezwe sera zitakazopunguza unyanyapaa na ubaguzi kazini. Alice Kariuki anaripoti

(SAUTI YA  ALICE KARIUKI)

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter