Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama Laongeza Muda wa Shughuli za UNSMIS

Baraza la Usalama Laongeza Muda wa Shughuli za UNSMIS

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, limeazimia kwa kauli moja kuongeza muda wa shughuli za waangalizi wa Umoja wa Mataifa nchini Syria, UNSMIS kwa kipindi cha siku 30 zaidi, na ambacho kitakuwa cha mwisho.

Kura ya leo ya kuongeza muda wa shughuli za UNSMIS, imeelezewa kama yenye ufanisi mkubwa, kufuatia hasa kukataliwa kwa mswada ambao ulikuwa na lengo la kukomesha umwagaji damu na kuzifanya pande zote katika mzozo wa Syria kuwajibika kwa ukiukaji wa haki za binadamu na mwongozo wa mpango wa amani wa Kofi Annan, wenye vipengee sita.

Mkuu wa UNSMIS Meja Jenerali Robert Mood, alisitisha shughuli za waangalizi hao hivi karibuni, kwa sababu ya mazingira ya hatari yalotokana na kuongezeka kwa ghasia nchini humo. Kufuatia azimio la leo, serikali ya Syria imepewa wajibu wa kuhakikisha usalama wa waangalizi wa UNSMIS.