Naibu Katibu mpya ataja Vipaumbele vyake Kwenye UM

20 Julai 2012

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Jan Eliasson ametaja vipaumbele anavyokusudia kuvipigua upatu wakati wa utumishi wake kwenye chombo hicho akitaja maeneo kama maendeleo na masuala ya kisiasa kuwa ndilo zingatio lake kuu.

Naibu Katibu huyo ambaye amekabidhiwa wadhifa huo hivi karibuni hata hivyo siyo mgeni sana katika utendaji wa chombo hicho na yeye amesema kuwa kukabidhiwa wadhifa huo ni kama vile kurejea nyumbani.

Amepata kushika nyadhifa mbalimbali kwenye Umoja wa Mataifa ikiwemo ile inayohusika na masuala ya usamaria mwema, rais wa baraza kuu na mjumbe maalumu huko Darfur nchini Sudan.

Mwanadiplomasia huyo kutoka nchini Sweden amehaidi kuchapa kazi licha ya kukabiliwa na changamoto za hapa na pale.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud