Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu Haki ya Kuwa na Maji na Usafi aelekea Kiribati

20 Julai 2012

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki ya kuwa na maji na usafi Catarina de Albuquerque anaendelea na ziara yake kwenye eneo la Pacific ambapo anatarajiwa kuizuru Kiribati kuanzia tarehe 23 hadi 26 mwezi huu kukagua haki ya haki za bidamu kuhusu maji na usafi.

Ziara yake ndiyo ya kwanza kufanywa na mtaalamu huru kutoka kwa baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa nchini Kiribati. Mtaalamu huyo ambaye anafanya ziara kwa mwaliko wa serikali ya Kiribati anasema kuwa ataangazia zaidi masuala la uhaba wa maji na usafi na pia athari za mabadiliko ya hali ya hewa. Wakati wa ziara hiyo yake ya siku nne mjumbe huyo atakutana na waakilishi kutoka kwa serikali na pia kutoka mashirika ya kimataifa na wafadhili ambapo pia atatembelea jamii kadha, vijiji na shule kabla ya kuwatubia waandishi wa habari.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter