Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Katiba mpya nchini Tunisia ni lazima izingatie haki za binadamu

Katiba mpya nchini Tunisia ni lazima izingatie haki za binadamu

Naibu mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Wha Kang kwa sasa anashiriki kwenye shughuli zinazohusu mazungumzo kuhusu katiba, sheria na haki za binadamu nchini Tunisia. Ofisi ya kamishina wa haki za binadamu nchini Tunisia imekuwa ikishirikiana kwa karibu na serikali pamoja na mashirika ya umma kuhusu mazungumzo hayo.

Kang amesisitiza kuwa katiba mpya ni lazima iwe na msingi dhabiti wa haki za binadamu ikiwemo haki ya kisiasa, kijamii na Kitamaduni kumbatana na matakwa ya watu wa Tunisia walioingia mitaani mwaka uliopita na kuwa na ushawishi mkubwa eneo hilo na mbali.